Wednesday, January 11, 2017

PATA KITABU CHA KAMPENI


Mwanaharakati Mayrose Kavura Majinge kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wameandaa Kampeni Maalum ya Kuinua Maadili Kitaifa itakayofanyika kuanzia mwezi Januari hadi Disemba 2017 kwa lengo la kuinua na kudumisha maadili ya Watanzania ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazodhoofisha mfumo wa muundo wa jamii yetu ya Kitanzania. 

Kampeni hiyo itaendeshwa kwa njia ya midahalo, usaili, tafakari kwa kutilia mkazo maelezo ya kitabu kiitwacho: “Chombo Muhimu kwa Maendeleo Yako” 

Uzinduzi huo utafanyika: Tarehe: 14 Januari, 2017 Muda:
Saa 9:00 Alasiri – 10:00 jioni 

Mahali: 6733 New Hempshire Avenue, 
Takoma Park, MD 20912 

 Lengo la Kampeni: Kuinua maadili mema kwa ajili ya kujenga mfumo bora katika kuendesha maisha yetu ya kila siku. 

 Kauli Mbiu ya Kampeni:Maadili mema na mfumo bora katika jamii vinaanza na mimi na wewe, tujielekeze kwenye ukweli huu tujenge maisha yenye tija” 

Habari zaidi piga namba: 

Habari zaidi PIGA 703 981 1323 

Tanzania itajengwa na watanzania.Karibuni sana.

No comments:

Post a Comment