Tuesday, December 19, 2017

Angalia Video: Sifa za Rais wa Tanzania Zatajwa - Part one & two



KILELE CHA AWAMU YA KWANZA YA KAMPENI YA KUINUA MAADILI KITAIFA TAREHE 10 DESEMBA 2017

Ndugu Wadau wa Kampeni;
Ndugu Watanzania Wenzangu;
Mabibi na Mabwana;

Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kufika siku hii ya leo; na kwa kutujalia pumzi na nguvu kwa kipindi chote cha mwaka huu tangu tulipozindua Kampeni hii ya Kuinua Maadili Kitaifa Januari hadi leo Disemba 2017.

Pia, nichukue fursa hii kuwashukuru wote walio ndani na nje ya nchi kwa kushiriki kampeni hii.
Vilevile, niwashukuru sana na kuwapongeza; wadau wote kutoka ndani na nje ya nchi waliojitoa kwa hali na mali kuchangia mahitaji ya kampeni hii. Wameonyesha moyo wa uzalendo wa hali ya juu sana kwani kuunga mkono suala la maadili ni kuunga mkono sekta zote za maandeleo ya jamii katika Taifa. Kitendo hiki kimeonyesha unyeneyekevu na upendo wa dhati kwa taifa letu. Tunaamini mbegu ya mwenendo kama huo wa moyo uzalendo wa kweli ni uthibitisho kuwa; pamoja na tatizo kubwa la mmomonyoko wa maadili uliokithiri nchini na duaniani kwa ujumla, bado nyumbani kwetu Tanzania tuna watu wenye maadili mema ambao wakithaminiwa na kuenziwa; tutaweza kulijengea taifa mfumo hai na kuliondoa katika mfumo mfu usiojali utu, upendo na umoja wa kitaifa. 
Na mwisho ila kwa umuhimu wa pekee, ninawashukuru ninyi nyote mlioacha shughuli zenu na kushiriki katika maadhimisho haya siku ya leo. Mwenyezi Mungu awabariki sana na kuwajaalia maisha marefu yenye tija na furaha.

Ndugu Watanzania Wenzangu;

Tarehe 14 Januari, 2017 Mwanaharakati Mayrose Kavura Majinge kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo waishio Marekani waliandaa na kuzindua Kampeni Maalum ya Kuinua  Maadili Kitaifa ambayo leo tunaadhimisha kilele cha Awamu ya kwanza.

Lengo  Kuu la Kampeni hii ni  Kuinua maadili mema kwa ajili ya kujenga mfumo bora katika kuendesha maisha yetu ya kila siku.

Kampeni hii iliendeshwa kwa njia ya Midahalo, Shindano la Hoja, Usaili na tafakari kwa kutilia mkazo maelezo ya kitabu cha Kampeni kiitwacho: “Chombo Muhimu kwa Maendeleo Yako”


Kauli Mbiu ya Kampeni: “Maadili mema na mfumo bora katika jamii vinaanza na mimi na wewe, tujielekeze kwenye ukweli huu tujenge maisha yenye tija”

Ndugu Watanzania wenzangu;
Kampeni hii iliendeshwa kwa kutumia vyombo vya habari kwa lengo la kuwafikishia ujumbe Watanzania wote waishio ndani na nje ya nchi yetu.
Vyombo vya habari vilivyojitoteza kusambaza ujumbe wa kampeni hii ni mitandao ya kijamii zikiwemo Blogs ambapo tuna blog ya kampeni hii: www.maadilikitaifa.blogspot.com ; Youtube; WhatsApp; Emails; Facebook; twitter; Instagram, pamoja na usambazaji wa kitabu cha kampeni sehemu mbalimbali nchini.
Tunawashukuru sana wanahabari na wadau wote walioshiriki katika awamu ya kwanza ya kampeni hii muhimu kwa mstakabali wa Maendeleo ya Taifa letu. 
Ushiriki wenu umeonyesha moyo wa uzalendo.

Thursday, February 9, 2017

Mbinu Mpya ya Kupambana na Ufisadi na Maovu Mengine Yaanza Kutumika

Mtaalam wa Maendeleo ya watu Mayrose Kavura akiwa pamoja na baadhi ya Watanzania waishio Marekani katika Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa 2017, Maryland Marekani.
 

Sunday, February 5, 2017

Mayrose pamoja na Baadhi ya Watanzania Waishio Marekani Katika Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa 2017, Maryland Marekani.

Mtaalam wa Maendeleo ya Watu Mayrose Kavura Majinge akieleza umuhimu wa Kanuni ya Dhahabu "The Golden Rule" Katika kuondoa Ufisadi na maovu mbalimbali katika jamii yetu. Fuatilia Habari kamili: maadilikitaifa.blogspot.com


Profesa Nicholls Boas wa Chuo Kikuu Maryland Marekani akiwa miongoni mwa wadau Watanzania waishio Marekani akifurahia jambo wakati wa Siku Maalum ya Kuwezesha Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa iliyofanyika Katika ukumbi wa Quality One Care, Maryland Marekani.



Baadhi ya wadau wa Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa kutoka maeneo mbalimbali nchini Marekani wakifuatilia kwa makini Maudhui ya Siku Maalum ya Kuwezesha Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa iliyofanyika Katika ukumbi wa Quality One Care Silver Spring, Maryland Nchini Marekani.

Saturday, January 28, 2017

MPANGO WA KUFANIKISHA KAMPENI YA KUINUA MAADILI KITAIFA JANUARI – DISEMBA 2017

Kauli mbiu ya Kampeni: “Maadili mema na mfumo bora katika jamii vinaanza na mimi na wewe, tujielekeze kwenye ukweli huu tujenge maisha yenye tija”


KAMPENI MAALUM YA KUINUA MAADILI KITAIFA JAN - DEC, 2017

Kiongozi wa Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa Bi Mayrose Kavura Majinge, siku ya Jumamosi Jan 14, ameweza kushirikiana na wadau mbali mbali jijini hapa Washington kwa lengo la kuinua Maendeleo Maalum ya Maadili Kitaifa, yaliyoanza rasmi kufanyika mwezi huu Januari hadi Disemba 2017, kwa lengo la kuinua na kudumisha maadili ya Watanzania ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazodhoofisha mfumo wa muundo wa jamii yetu ya Kitanzania.